SIASA ZA KITAIFA
kinara wa chama cha wiper kalonzo musyoka amesema kwamba ana imani kuwa kwa ushirikiano na viongozi wengine watambandua afisini rais dkt william ruto
kwa kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
akiongea kwenye eneo bunge la likoni katika kaunti ya mombasa, kalonzo
ameusuta uongozi wa rais ruto akisema kwamba umefeli kushughulikia
maslahi ya wananchi kama walivyokuwa wameahidi.
kalonzo ameongeza kwamba sekta muhimu kama vile afya na elimu zimeendelea
kukumbwa na changamoto kutokana na sera mbovu zilizoanzishwa na serikali
ya kenya kwanza baada ya kutwaa mamlaka ya nchi.
Insert kalonzo on ukombozi.
KITAIFA
viongozi kwenye chama cha odm wameendelea kukariri kwamba chama hicho hakijaingia katika serikali ya kenya kwanza kufuatia kuteuliwa kwa baadhi ya wanachama wake kama mawaziri.
mbunge wa suba kaskazini millie odhiambo amesema kwamba chama hicho
kinaendeleza ushirikiano na serikali kwa ajili ya kuboresha utendajikazi kwa
manufaa ya wananchi.
kulingana na odhiambo ambaye ni kiranja wa walio wachache bungeni ni
kwamba kufikia sasa hakuna mkataba wa kuingia serikalini uliotiwa saini baina ya chama cha chungwa na utawala wa kenya kwanza.
Insert odhiambo on serikali..
BUNGOMA
maafisa wa usalama kwenye eneo la bungoma kaskazini wameimarisha msako dhidi ya watu majambazi waliomwangamiza mlinzi wa shule ya upili ya
namboko wiki iliyopita.
akiongea kwenye mkutano wa kiusalama mkuu wa polisi eneo hilo sammy
kosgei hata hivyo amewahimiza wananchi kushirikiana na maafisa wa usalama kwa kutoa taarifa muhimu.
kosgei amesema kuwa taarifa kutoka kwa wananchi utasaidia katika
kufanikisha uchunguzi utakaosaidia kuwabaini waliohusika na mauwaji ya
kinyama ya mlinzi huyo.
Insert kosgei on usalama
aidha naibu kamishna eneo hilo martin mureithi amekariri kwamba
watahakikisha waliohusika na mauwaji ya mlinzi huyo wanakamatwa na
kuchukuliwa hatua za kisheria.
Insert mureithi on washukiwa
trans nzoia
jumla ya shule tano za msingi katika kaunti ya trans nzoia zinatarajiwa kufaidi na vitabu vya kusoma vilivyotolewa kupitia kwa ufadhili wa wahisahi kutoka
kwenye kundi la giants group of nairobi twiga.
akiongea baada ya kupokea vitabu hivyo vyenye dhamani ya shilingi milioni
mbili, gavana george natembeya amesema kwamba ufadhili huo utairamisha uwezo wa wanafunzi kusoma na hivyo kuimarika kimasomo.
aidha kwa upande wao wahisahi hao akiwamo mkuu wa kundi hilo nakesh besai na mkewe chetna besai, wamewataka wazazi kuhakikisha kwamba wanao
wanasoma wakati wako nyumbani kando na kuzingatia nidhamu.
Insert natembeya on kusoma.
POKOT MAGHARIBI
gavana wa kaunti ya pokot magharibi simon kachapin ametangaza kuwa
wafanyabishara wanaoendesha shughuli zao katika soko la bendera eneo la kapenguria hawatahitajika kulipa ushuru kwa mwaka moja.
akiongea kwenye hafla ya ufunguzi wa soko hilo, gavana kachapin amesema
hatua hiyo itahakikisha wafanyabishara hao wanajimudu mwanzo kabla ya kuanza kulipa kodi.
aidha gavana kachapin ameahidi kwamba utawala wake utaendelea kuimarisha mazingira ya biashara kwa afanyabishara ili kuwapa nafasi ya kuendeleza shughuli zao bila changamoto.
Insertt kachapin on kodi
KIMATAFA.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ametishia kujitoa kwenye makubaliano ya kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza.
Netanyahu ameyaagiza majeshi yake kujiandaa kuanzisha tena mashambulizi dhidi ya Hamas ikiwa hawatawaachia mateka zaidi siku ya Jumamosi.
Hamas ilisema siku ya Jumatatu na kurudia jana Jumanne kwamba pengine watasogeza mbele muda wa kuwaachilia mateka watatu wa Israel wakiishutumu kwa kushindwa kukidhi masharti ya makubaliano ya kusitisha mapigano.
Rais Donald Trump wa Marekani baada ya kukutana na Mfalme Abdullah II wa Jordan kwenye Ikulu ya White House siku Jumanne, alielezea mashaka yake ikiwa Hamas watawaachilia mateka wote waliosalia kama ambavyo amekuwa akishinikiza.
Show quoted text
Comments
Post a Comment