MAONI YA WAKAZI WA TRANS NZOIA KUHUSU UAMUZI WA TRUMPH
Maoni ya wakazi kuhusu kauli ya rais wa marekani Donald Trumph
Siku chache baada ya rais wa marekani Donald trump kuapishwa amesema kuwa ni wakati sasa viongozi wa nchi zingine kuacha ufisadi na kuanza kujitegemea .wakazi wa kaunti ya trans nzoia wametoa kauli mbalimbali kuhusiana na hoja hiyo ya trump
kulingana na barrack mkaazi wa mji wa kitale katika kaunti ya trans nzoia amesema kuwa Trump amekosea kusema kuwa viongozi wa afrika wajisimamie kwa sababu marekani wakiwa wafadhili wakuu wanapaswa kushiriakiana na viongozi wa nchi ambazo hazijaendeleai ili kuwainua kimaendeleo .
kauli sawia imekaririwa na junephana wepukhulu mkaazi wa liyavo amemwomba trump kutositisha ufadhili wa madawa kwa sababu watu wenye maisha ya chini ambao wanaoishi na virusi vya ukimwi, saratani na malaria ndio watakaongamia kwa kukosa fedha za kufadhili matibabu Yao.
Aidha, Boaz khaemba ambaye ni bodaboda wa mji wa kitale amesema kuwa anaunga hatua ya trump ya kuondoa misaada kwa sababu misaada mingi inayotakona na ufadhili wa marekani uwa unaishia kwa mikono ya viongozi fisadi nchini bila kufikia mwananchi wa kawaida.
Comments
Post a Comment