MUUNGANO WA KISIASA
katika hafla ya uzinduzi wa chama Cha DAPK,Aliyekuwa naibu wa rais Rigathi gachagua,kinara wa wiper democratic kalonzo musyoka na Eugene wamalwa wa DAPK wameahidi kuungana mkono KISIASA ili kumuondoa rais Ruto mamlakani ifikapo mwaka wa 2027.
Akizungumza na wanahabari kwenye hafla hiyo Rigathi amewaonya wakenya dhidi ya kumrudisha mamlakani rais Ruto kwa awamu ya pili.Amewarai pia wakazi wa eneo pana la magharibi wasidanganywe na rais kwani watasalitiwa .
kauli sawia imekaririwa na kinara wa wiper kalonzo musyoka amesema kuwa watashirikiana ili kumng'atua uongozini rais Ruto.
Aidha Eugene wamalwa amekiri kuwa wako tayari kwa kivumbi Cha kisiasa Cha mwaka wa 2027 ili kuleta mabadiliko nchini
Comments
Post a Comment